Monday, 14 March 2016

SMZ kushughulikia wahalifu

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema itapambana na watu wanaofanya matukio ya hujuma ikiwemo kuharibu huduma za jamii kwa wananchi. Aidha, watu wawili wanashikiliwa na Polisi kisiwani Pemba kwa uchunguzi zaidi kutokana na kutuhumiwa kuhusika na uchomaji moto kwa nyumba za wakazi pamoja na kituo cha afya na tawi la CCM Tibirinzi.
0 Comments

Ndalichako: Mikopo ya HESLB ilipwe

SERIKALI imeendelea kuwasisitiza Watanzania walionufaika kwa mikopo ya elimu ya juu kurejesha fedha walizokopa ili wengine wanufaishwe nayo pia. Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisisitiza hivyo hivi karibuni, alipokuwa akizungumza na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St Joseph cha Dar es Salaam waliogoma kuingia darasani kwa sababu mbalimbali.
0 Comments

Mkwasa aagiza watumishi wazembe kutumbuliwa

MKUU wa Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, Betty Mkwasa, amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, kuchukua hatua za haraka kwa watumishi waliosababisha jengo la vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Sekondari Wami kushindwa kutumika.
0 Comments

No comments:

Post a Comment